Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amemuongelea mchezaji wake Darwin Nunez ambaye wamemsajili msimu huu kutoka Benfica na kusema kuwa anafanya jitihada kubwa sana mazoezini.

Klopp amesema kuwa Nunez anahitaji kujituliza, lakini mienendo yake ni ya kipekee, anahitaji kuendelea kujituma klabuni hapo kwani Liverpool anapitia wakati mgumu kwasasa toka apate majeraha.
Nunez amejiunga na Liverpool akitokea Ureno katika klabu ya Benfica huku katika michezo 57 aliyocheza amepata magoli 32, na kutoa pasi za mabao 13 klabuni huko. Na sasa yupo Anfield kwa Jurgen.

Liverpool inatarajiwa kutua dimbani hapo kesho dhidi ya Arsenal, ambapo The Gunners ndio vinara wa msimamo EPL, wakati Majogoo wapo nafasi ya 9 huku tofauti ya pointi kwao ikiwa ni 11.

