Kawaida ya soka lazima kuwe na ushindani, na kila timu huwa inahitaji kufanya vizuri zaidi ya nyingine! Ili hii iweze kutokea lazima wawepo wa kushinda na wakupoteza gemu kwa nyakati tofauti, huwa ni ahueni kwa klabu fulani kuon a inajiweka katika gepu kubwa la tofauti ya pointi mbele ya mpinzani wake! Hebu tuone majibizano ya meneja Jurgen Klopp na mlinzi wa Manchester City Kyle Walker.
Chanzo cha majibizano
Liverpool na Manchester City ndiyo klabu zinazofukuziana kwa ukaribu sana kama vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu wakiwa na tofauti ya pointi tano tu kwa sasa. Gemu zilizopita, Machester City walichezea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Newcastle. Liverpool wakawa na gemu siku inayofuata dhidi ya Leicester City, na wao wakakaziwa na kulazimisha sare ya 1-1 kwa wageni wao. Kama Liverpool wangeshinda basi wangekuwa wanaongoza ligi wakiwa na pointi 7 mbele ya Manchester City.
Baada ya gemu ya Liverpool, Kyle Walker alichapisha picha ya Harry Migure akiambatanisha ujumbe unaotafsirika kuwa “Kwa hiyo, walifikiri wangekuwa na pointi 7 mbele (yetu)…” Licha ya Walker kufuta chapisho lake, chapisho hilo tayari lilivuma ndani ya mda mfupi kwenye mitandao .
Majibu ya Klopp
Klop alipoulizwa kuhusu ujumbe huo amejibu kuwa, licha ya kuwa yeye hapendi kufuatilia nini kinaandikwa sana na mastaa kwenye mitandao ya kijamii, lakini hajawahi kushangilia timu nyingine inapopoteza pointi. Kwake yeye anaamini hiyo haitakiwi kuwepo, anasema labda hiyo ingekuwa kwa mashabiki huko sio kwa wahusika kama wao.
Liverpool na Manchester City wanatofautiana kwa pointi 5 huku wakiwa na gemu 14 mezani mpaka mwisho wa ligi hii! Gemu zilizobaki zitaendelea kuthibitisha nani ni mtabe kwa mwenzie!


Furahav
Klopp iko vizuri.
Issa
Kloop katumia busara kubwa kama kocha
Povel
Gud news