MARCELO LIPPI: Kocha Mkongwe Aliyezalisha Makocha wa Kipindi Hiki

Kua na wachezaji wazuri na bora haikufanyi uwe na timu bora ila mifumo na mipango ndio kila kitu, kupitia huo mfumo na mbinu zako kwanza kabisa utafanya mchezaji watumie kila chembe ya uwezo wao kwa ajili ya timu pili utamfanya mchezaji afurahie game na mengine mengi.

Italy haijawahi kuyumba kutuletea vichwa vya mpira tena vinakua World Class. Kina Arigo Sacchi , Fabio Capello, Antonio Conte , Masimilliano Allegri, Carlo Ancelloti, Marcelo Lippi, Sarri na wengine wengi. Marcelo Lippi..

Italy kule ndiko linapatikana soka la kilinzi kama ni kulinda tu kule umefika, kuna stori ilisambaa kwamba Giorgio Chellini na wenzake walihitaji goli moja tu kuitoa Barca, kwamba walikua na uwezo wa kuwazuia MSN kwa mechi mbili bila kuruhusu goli.

 

Marcelo Lippi kilikua kichwa kingine kutoka Italy na kilikuja na usataratibu wake na kuchukua makombe yake likiwemo la dunia , siku zote utamu wa makocha huja katika mbinu zao na namna ya uongozi wao.

Lippi alitawala kwa mifumo ya kigumu sana alitumia sana 4-4-2 na 4-5-1 ( hii 4-5-1 ina weza kua 4-2-3-1 au 4-2-3-1 au 4-1-4-1 ) na( huu wa 4-4-2 unaweza kuja na 4-4-1-1 ). Marcelo Lippi hakutoka nje ya hapa kabisa , atabadilika kulingana na hali ya mechi na mpinzani wake.

Marcelo Lippi

Dunia ilianza kufaidi shoo za huyu mzee baada ya kuipaisha sana na kuipeleka Napoli michuano ya UEFA msimu wa 1993/1994, Juventus wakamtwaa kama unavyojua mwenye kisu kikali ndo hula nyama nyingi kule alikutana na minofu ivo alikula sana makombe Ginaluca Vialli , Roberto Baggio , Alsandro Del Piero , Didier Deschamps , Antonio Conte na wengine wengi.

Aliwakosha watu wa mpira baada ya ujio wa Zinadine Zidane mwaka 1996, ikumbukwe alikua anatumia 4-3-3 lakini akahamia kwenye 4-4-2 hii ilitokea sababu Zidane alikua kiungo mshambuliaji anayetokea katikati ivo ilibidi abadilike tu, jamaa akaja na 4-3-1-2 huyo mmoja hapo ndo alikua Zidane .

Marcelo Lippi hakukariri maisha wala hakukariri mifumo na alibadilika kulingana na mpinzani na aina ya mechi pia aina ya wachezaji alionao, pale Ujerumani katika kombe la dunia 2006 alidunda karibu na mifumo kadhaa kuna watu aliwapiga na 4-5-1 tena wapo waliofia katika 4-4-2 au 4-4-1-1.

Jamaa kama atakumbana na timu zinazoshambulia kwa kasi basi 4-4-2 ilikua kimbilio lake mfano ilikua mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani

Marcelo Lippi atakumbukwa sanaa sio tu kwa uwezo wake wa kufundisha pia uongozi wake ulikua mzuri, ikumbukwe mkononi wamepitia makocha wazuri tu kama Antoine Conte, Zinadine Zidane, Didier Deschamps na wengine wengi.

Italy ni kama kitako cha soka mifumo na mbinu nyingi za utawala zimetumika sanaa kule , inaweza isiwe ligi inayovutia pia haina mashabiki wengi lakini ni moja ya nchi zilizoleta mapinduzi makubwa katika soka. Soka ni kama somo la uchumi huwezi kulifafanua kwa namna moja, ndio maana zimekuja mbinu nyingi sanaa mpaka leo.

20 Komentara

    Thanks meridian bet tz kwa update za kisport na burudani

    Jibu

    Huyu babu aliasumbua ulimwengu wa soka

    Jibu

    Alikuwa anafanya vizuri Sana enzi zake

    Jibu

    Huyu Babu ujana wake alikuwa
    Yuko vizuri sana kwenye ulimwengu
    Wa soka

    Jibu

    Good news 👍#meridianbettz

    Jibu

    Nice article #meridianbettz

    Jibu

    huyu mzee alikua hana mpinzani

    Jibu

    He is a true Legend, Kweli jamaaa kaleta makocha wengi sana kutokea kwenye Falsafa zake.

    Jibu

    Coach mwenye uwezo mkubwa…asante meridianbettz kwa habari za michezo nzuri.

    Jibu

    Bado hanamfano wa kuigwa..!marcelo

    Jibu

    mfano wa kuigwa kocha mkongwe ndo mana makocha wengi weng wamemfata

    Jibu

    Ni Kocha mwenyew uwezo mzur sana ametisha

    Jibu

    Huyu Babu alikuwa anafanya vizuri enzi yake

    Jibu

    Huyu kocha anaujuzi Sana Ndio maana makocha wengi Sana wamemfuata kwenye ukocha

    Jibu

    Asante kwa habari safi.

    Jibu

    KochA mkongwe mwenye mbinu matata sana za ufundishaji

    Jibu

    Namkubali ile mbaya

    Jibu

    Hongera sana kocha wa ulimwengu.

    Jibu

    saf

    Jibu

    Hakika alikuwa Kocha makini sana na anakuwa mzuri zaidi pale watu wanapoiga mbinu zake #Meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe