Maresca Ataka Usajili Wa Beki Kufidia Pengo la Colwill

Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, amesisitiza kuwa klabu inapaswa kusajili beki wa kati mpya kuziba pengo lililoachwa na Levi Colwill, ambaye atakosa sehemu kubwa ya msimu mpya baada ya kuumia goti akiwa mazoezini.

Maresca Ataka Usajili Wa Beki Kufidia Pengo la Colwill

Beki huyo wa kimataifa wa England, mwenye umri wa miaka 22, alikuwa sehemu muhimu ya safu ya ulinzi ya The Blues msimu uliopita, hasa katika ujenzi wa mashambulizi kutoka nyuma. Maresca amekiri kuwa anatafuta suluhu ndani ya kikosi cha sasa, lakini amebainisha wazi kuwa klabu inajua maoni yake kuhusu umuhimu wa kuongeza beki mpya.

“Tulieleza mara nyingi jinsi Levi alivyo muhimu kwetu msimu uliopita, hasa kwa namna tunavyotaka kucheza,” alisema Maresca. “Tunaweza kuunda nafasi na kushambulia kwa njia sahihi iwapo tutajenga mashambulizi kwa mpangilio sahihi. Levi alikuwa sehemu kubwa ya mpango huo, na sasa hayupo. Tunaangalia suluhu za ndani, lakini klabu inajua nilichosema. Nadhani tunahitaji beki wa kati.”

Maresca Ataka Usajili Wa Beki Kufidia Pengo la Colwill

Katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Jumapili dhidi ya Crystal Palace, Tosin Adarabioyo na Trevoh Chalobah wanatarajiwa kuanza kama mabeki wa kati. Hata hivyo, Chelsea imehusishwa na tetesi za kumtaka Antonio Silva kutoka Benfica kama mbadala wa muda mrefu wa Colwill.

Licha ya kauli ya kocha wa Liverpool, Arne Slot, kwamba Chelsea ni miongoni mwa wapinzani wakuu wa ubingwa, Maresca amekataa kuingia kwenye michezo ya kisaikolojia na makocha wenzake. “Sijali wanachosema wengine kuhusu sisi,” alisema Muitaliano huyo. “Sipendi kucheza michezo ya maneno, napenda kuzingatia wachezaji na kuendelea kuboresha timu.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Maresca Ataka Usajili Wa Beki Kufidia Pengo la Colwill

Chelsea inaanza msimu huu katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kurejea mazoezini muda mfupi uliopita kufuatia mafanikio yao ya kushinda Kombe la Dunia la Klabu. “Tunaamini tupo tayari,” alisema Maresca. “Ni mapumziko mafupi, lakini tumejitahidi kujiandaa. Hii ni hali mpya, na kwa kweli hatuna majibu ya moja kwa moja kwa sababu ni jambo jipya kwetu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.