Nani Alistahili Heshima?

 

Pongezi ni kitu ambacho kila mmoja hupenda kufanyiwa pale anapoonekana kufanya jambo fulani au kitu fulani kwa mafanikio makubwa. Jambo hilo mara nyingi huchochea utendaji kazi na mara nyingi huwafanya na wengine kuchukua fursa hizo kuangalia namna wanavyoweza kupambana ili kupata nafasi ya kupongezwa.

Kama ilivyo heshima ndani ya ligi kuu ya Uingereza kwa mchezaji kutambulika nafasi yake uwanjani na makubwa anayoyafanya, basi hata mwalimu wake hupata nafasi ya kupewa kila kinachoonekana kama hongera kwa kuipa timu yake mafanikio fulani au kuifikisha katika hatua fulani yenye mafanikio.

Hivyo basi, katika nafasi hiyo ligi kuu ya Uingereza iliweka mezani makocha watatu ambao walishindanishwa juu ya nani amefanya vema sana katika msimu huu wa ligi kwa kipindi cha mwezi wa pili. Makocha hao ni Guardiola wa Man City, Ole wa United na Emery wa Arsenal.

Pep Guardiola

Kabla ya kuingia Februari, Liverpool walikuwa alama tano mbele yao lakini kadri wakati unavyozidi kusonga mbele, timu hiyo sasa imeonekana kurejea juu tena baada ya kucheza soka safi lenye kuonesha nia yao kubwa ni ipi ndani ya michuano hiyo kuelekea taji la ligi hiyo. Mwezi Februari umemwendea vizuri zaidi mara baada ya kushinda mechi zake nne za ligi hiyo kwa idadi kubwa ya magoli, huku mchezaji wake Arguero akiwa ametajwa kama mchezaji bora wa mwezi.

Ole Gunnar Solskjaer

Ni ukweli usiopingika ametua United akiwa na damu ya klabu hiyo kitu ambacho hadi sasa kinampa nafasi kubwa sana ya kuendelea kuwa bora kwa nafasi yake. Kwa mwezi Februari ameshinda mechi zake tatu huku akitoka suluhu na Liverpool pekee. Amejua namna ya kukitumia kikosi hicho kwa sasa pamoja na idadi kubwa sana ya majeruhi alionao lakini haijaweza kuwa kikwazo kwake kuondoka na matokeo kadri anavyotaka yeye.

Unai Emery

Naye anaungana na wenzake kuelekea kuonesha ubora aliokuja nao ndani ya klabu yake hiyo huku katika takwimu akiwa ameshinda mechi zake tatu kati ya nne alizozicheza mwezi Februari akipoteza mechi yake moja mbele ya Guardiola. Kwa sasa anaenda kukutana na United mara baada ya kutoa sare na Spurs kwenye mechi yake ya mwishoni mwa wiki.

Mchuano mkubwa wa nafasi hii ulikuwa kwa vinara wawili ambao ni Guardiola na Ole ambao kwa hakika wanaonekana kufanya vizuri zaidi ndani ya mechi zao wanazocheza uwanjani, na Ole akajizolea alama zaidi kutokana na alipoitoa timu hiyo hadi sasa japo wanazidiana na hatimaye Pep kutwaa ushindi!

 

3 Komentara

    Ni sawa jambo jema.

    Jibu

    Ni kweli kabisa

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.