Frenkie De Jong Amkosha Xavi

Kiungo wa klabu ya Fc Barceloba Frenkie De Jong amemkosha kocha wa klabu hiyo Xavi Hernandez kutokana na kiwango bora ambacho amekua akikionesha klabuni hapo.

Kiungo Frenkie De Jong ambaye amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu ya Barcelona huku klabu ya Manchester United ikihusishwa zaidi na mchezaji huyo, Lakini kiungo huyo ameonesha ubora mkubwa zaidi ndani ya klabu hiyo msimu huu.frenkie de jongKocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez wakati anafanya mahojiano na wanahabari alisema “Tumeona ubora wa De Jong tangu mimi na wasaididzi wangu tumefika hapa. Frenkie anafanya kazi kubwa kwenye kushambulia na kuzuia, Amekua anajiamini kwa kiwango kikubwa na tunafurahia hilo”

Kiungo huyo licha ya kuonesha ubora mkubwa ndani ya klabu ya Barcelona lakini bado taarifa zinaeleza kua mchezaji huyo huenda kauzwa ndani ya klabu hiyo, Na hiyo ni kutokana na matatizo ya kiuchumi ambayo yanawakabili klabu ya Fc Barcelona.frenkie de jongKiungo Frenkie De Jong amepokea sifa nzuri kutoka kwa mwalimu wake Xavi Hernandez ambaye mwanzo ilionekana kama hampi muda wa kutosha kiungo huyo, Lakini kwasasa inaonekana kocha huyo amekubali kazi iliyotukuka ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.