Kiungo wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Malaga, na Sevilla Isco Alarcon amefanikiwa kurudi uwanjani na kujiunga na klabu ya Real Betis kwa uhamisho huru.
Kiungo Isco alijiunga na klabu ya Sevilla baada ya kuondoka klabu ya Real Madrid majira ya joto msimu uliomalizika, Lakini alishindwa kuendelea klabuni hapo mwezi Januari na kutaka kujiunga na klabu ya Union Berlin ya nchini Ujerumani ambapo uhamisho huo ulikwama.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alikaa nje ya uwanja tangu mwezi Januari bila timu baada ya uhamisho wake kuelekea klabu ya Union Berlin kushindikana lakini kwasasa kiungo huyo atakuwepo uwanjani baada ya uhamisho wake kuelekea Real Betis kukamilika.
Kiungo Isco atajiunga na Real Betis kwa mkataba wa mwaka mmoja mpaka mwaka 2024, Huku akiwa ni kipaumbele cha kocha wa klabu hiyo Manuel Pelligrini ambaye amewahi kufanya kazi na mchezaji huyo akiwa Malaga.
Kiungo huyo fundi sasa atawatumikia Real Betis msimu ujao baada ya kukamilisha vipimo vya afya na klabu hiyo, Wengi wanaamini mchezaji huyo anaweza kufanya vizuri licha ya kuwepo nje ya uwanja kwa miezi sita kwani ubora wake unajieleza.

