Isco Akwama Kujiunga na Klabu ya Union Berlin

Kiungo wa zamani wa klabu ya Real Madrid Isco Alarcon amekwama kujiunga na klabu Union Berlin inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani baada ya dili lake kukwama dakika za mwisho.

Mchezaji Isco alikubaliana kila kitu na klabu ya Union Berlin na ilielezwa kilichokua kinasubiriwa ni kandarasi kusainiwa baina ya pande zote mbili, Na baadae ikaelezwa dili hilo kuvunjika kabla ya siku moja ya dirisha kufungwa.iscoMchezaji huyo alikua anajiunga na klabu ya Union Berlin kama mchezaji huru baada ya kumalizana na klabu ya Sevilla ambapo alidumu kwa muda wa miezi minne tu, Mchezaji huyo alidumu ndani ya miamba hiyo Hispania kwa miezi minne kabla ya kuvunja mkataba wa kuachana na klabu hiyo.

Mkurugenzi wa klabu ya Union Berlin amezungumza kwanini usajili huo umeshindwa kukamilika na kueleza kua walihitaji sana kupata saini ya mchezaji huyo lakini muda ulipitiliza na licha ya makubaliano ya awali lakini dili hili haliwezi kufanikiwa tena. Hii inaonesha kua muda wa usajili kwa upande wa Ujerumani uliisha kwa wachezaji wanaoingia hivo kumzuia Isco asiweze kucheza Union Berlin.iscoKwa upande wa mchezaji Isco Alarcon wao wameeleza kua mazungumzo ambayo walikubaliana na klabu hiyo mwanzoni yalivunjwa na kusababisha mchezaji huyo kubadilisha mawazo yake Hivo dili lake la kujiunga na klabu hiyo kuvunjika rasmi. Ni wazi kua mchezaji huyo alishindwana na klabu hiyo katika makubaliano binafsi kutokana na maelezo ya mawakala wake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.