Arsenal Wajitoa kwa Caicedo

Klabu ya Arsenal imejitoa katika dili la kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ecuador Moises Caicedo anayekipiga katika klabu ya Brighton and Hove Albion baada ya kumsajili Jorginho Frello kutoka Chelsea.

Washika Mitutu hao wa London walikua wakifukuzia saini ya kiungo Moises Caicedo kwa muda wa wiki moja lakini dili hilo halikuweza kufanikiwa mpaka klabu hiyo ilipoamua kuhamishia nguvu kwa aliyekua kiungo wa Chelsea Jorginho Frello.arsenalKlabu ya Arsenal katika hali ya kushangaza ilibadili gia angani baada ya kuhamishia nguvu kwa kiungo wa zamani wa Chelsea Jorginho na kuweza kumsaini nyota huyo, Na klabu hiyo ilifanikiwa kumsajili kiungo huyo fundi kwa mkataba wa miaka miwili mpaka 2024.

Klabu ya Brighton Hove and Albion nao wameendelea kushikilia msimamo wao wa kiwango cha pesa ambacho wanakihitaji kwa mchezaji huyo kwa klabu yeyote itakayomuhitaji Moises Caicedo. Klabu hiyo imekua ikihitaji kiasi cha Euro Milioni 60 ili kumuachia mchezaji huyo.arsenalKlabu ya Arsenal wamefanikiwa kumchukua Jorginho kutoka Chelsea baada ya kupiga chini dili la mchezaji Moises Caicedo kwenye dirisha hili la mwezi Januari, Lakini taarifa zinaeleza klabu hiyo itaendelea kumfatilia kiungo huyo kwani bado yupo kwenye mipango ya klabu hiyo ikiwezekana watarudi kwenye dirisha kubwa.

Acha ujumbe