Ac Milan na Leao Bado Wanajadili Mkataba Mpya

Klabu ya Ac Milan imekanusha juu ya taarifa za kuvunjika kwa mazungumzo ya mkataba mpya baina yao na mchezaji wake nyota raia wa kimataifa wa Ureno Rafael Leao.

Siku ya leo taarifa kutoka nchini Italia zilizuka kua mazungumzo baina ya klabu hiyo na mchezaji wake Rafael Leao yamevunjika. Kitu ambacho klabu hiyo imekikqnusha kwa nguvu kubwa na kusisitiza mazungumzo baina yake na mchezaji huyo bado yanaendelea.ac milanMchezaji Rafael Leao amekua kwenye mazungumzo na klabu yake hiyo kwa muda mrefu sasa wakijadili mkataba mpya ambao utaendelea kumbakiza nyota huyo ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu. Ikumbukwe mchezaji huyo mkataba wake utamalizika mwaka 2024 hivo miamba hiyo inataka kumuongezea mkataba mpya aendelee kubaki kwa muda mrefu.

Vilabu vikubwa mbalimbali brani ulaya vimekua vikihitaji saini ya mchezaji Rafael Leao kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu hiyo, Hali hiyo imekua ikiwapa presha kubwa Ac Milan na kutaka kumuongezea mkataba mrefu mchezaji huyo.ac milanKlabu kama Chelsea, Arsenal na Manchester City zote kutoka Uingereza zimekua zikihusishwa kuhitaji saini ya Rafael Leao, Hivo Ac Milan wanahitaji kumpa mkataba mpya ambao utamueka klabuni hapo kwa muda mrefu ili kuepusha presha kutoka kwenye vilabu hivo na vilevile ikitokea anataka kuondoka basi waweze kumuuza kwa gharama kubwa.

Acha ujumbe