Winga Jadon Sancho na mshambuliaji Anthony Martial watarejea kwenye kikosi cha Manchester United kesho katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Carabao dhidi ya klabu ya Nottingham Forest.
Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amethibitisha kua nyota wake hao wawili watarejea katika mchezo wa kesho nusu fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Nottingham Forest. Nyota hao ambao wamekosekana uwanjani kwa muda kidogo.
Jadon Sancho hajaonekana akiwa amevaa jezi ya klabu ya Manchester United tangu mwezi Oktoba mwaka jana alipopata majeraha, Lakini pia alipona na kuendelea na programu maalumu chini ya usimamizi maalumu ili kuweza kurejesha utimamu wake.
Mchezaji Anthony Martial yeye amekua akikumbwa na majeraha mara kwa mara ndani ya klabu hiyo, Kwani mchezaji huyo ameshaumia zaidi ya mara tatu msimu huu lakini atarejea ndani ya timu hiyo kwenye mchezo wa kesho wa nusu fainali ya kombe la Carabao.
Mashabiki wa klabu ya Manchester United wameonesha kufurahishwa na taarifa za kurejea kwa wachezaji Jadon Sancho na Anthony Martial kwenye timu hiyo, Lakini kocha wa klabu hiyo amesisitiza kiungo wake Scott Mctominay ataendelea kuwepo nje ya uwanja.

