Gavi Apewa Jezi ya Xavi Barcelona

Klabu ya Fc Barcelona imemkabidhi jezi namba 6 kiungo Pablo Gavi ndani ya klabu hiyo ikiwa ni moja ya jezi zenye heshima kubwa sana ndani ya klabu ya Barcelona.

Klabu hiyo imemkabidhi kiungo huyo jezi hiyo ambayo ilikua ikivaliwa na kocha wa sasa ndani ya klabu hiyo Xavi Hernandez ambaye alikua moja ya viungo bora sana ambao dunia iliwahi kuwatizama. Hivo Gavi kukabidhiwa jezi hiyo ni jambo kubwa sana kwake.GaviKiungo huyo mwenye miaka 19 tu amekua akifanya vizuri sana ndani ya klabu ya Fc Barcelona tangu alipopata nafasi kwa mara ya kwanza kucheza timu ya wakubwa, Na kiwango chake kimekua kikiimarika siku hadi siku na ndio sababu iliyofanya klabu ya Barcelona kumkabidhi jezi nzito kama hiyo.

Kiungo Gavi ambaye amekua akifanya vizuri ndani ya klabu hiyo sambamba na kijana mwenzake Pedri na muunganiko wao umekua ukiwavutia watu wengi na kufikia hatua ya kuwafananisha na muunganiko wa Xavi na Iniesta. Kwasasa viungo hao watakua wakivaa jezi namba sita na nane kwani Pedri alishaanza kuvaa jezi namba nane kw amuda sasa.GaviBaada ya Pablo Gavi kukabidhiwa jezi namba sita iliyokua ikivaliwa na Xavi na Pedri kuvaa jezi namba nane iliyokua ikivaliwa na Iniesta mashabiki wengi wa klabu ya Barcelona wanatarajia makubwa kutoka kwa vijana hao, Kwani wamekua wakiwafananisha na magwiji hao waliofanya vizuri ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.