Kiungo wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya soka ya Fc Barcelona Pablo Gavi huenda akaweka rekodi kma taanza mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Morocco kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia.

Kiungo Gavi amekua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya ya Uhispania chini ya mwalimu Luis Enrique. Kiungo huyo licha ya umri wake mdogo lakini amekua akionesha uwezo mkubwa katika michezo ambayo amekua kaipewa nafasi.gaviKinda huyo ataweka rekodi leo kama ataanza katika mchezo wa 16 bora dhidi ya Morocco na kijana mdogo zaidi kuanza kwenye hatua ya mtoano baada ya gwiji wa kibrazil Edison Arantes do Nascimento maarufu kama Pele.

Gavi mwenye umri wa miaka 18 na siku 123 atakua mchezaji mdogo zaidi kucheza michuano hiyo baada ya baada ya Pele kufanya hivo mwaka 1958 akiwa na miaka 17 na siku 249.Huku ikumbukwe Pele aliisaidia Brazil kubeba ubingwa wake wa kwanza baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa fainali dhidi ya Sweeden.gaviKiungo Pablo Gavira amekua akionekana kama mchezaji bora na atakaekuja kufanya vizuri sana siku za usoni kutokana na uwezo ambao amekua akiuonesha licha ya umri wake kua mdogo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa