Beki wa timu ya taifa ya Japan na klabu ya Arsenal Takehiro Tomiyasu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza amesema kiwango chake cha chini kwenye mchezo wao dhidi ya Croatia kilisababisha timu yake ya taifa kutolewa.

Timu ya taifa ya Japan ilitolewa katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Croatia katika hatua ya upigaji wa penati. Japan walipambana mpaka hatua ya upigaji wa penati baada ya kucheza dakika 120.tomiyasuTakumi Minamino,Kaoru Mitoma na nahodha Maya Yoshida walikosa mikwaju yao ya penati iliyochomolewa na golikipa wa Croatia Dominik Livakovic na kuifanya Japan kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia.

Beki huyo alieleza “Kiwango changu kilikua kibovu samahani kwa timu. Nilitakiwa kufanya zaidi ili kuisaidia timu. Kiwango changu na cha timu hakikua vizuri, Tulihitajika kupambana zaidi Japo tulikaribia kufanikiwa ila walikua bora kuliko sisitomiyasuTomiyasu ambae alikua na wastani mbovu zaidi katika upigaji wa pasi katika mchezo huo ambao alicheza dakika 120 huku pia akiongoza kwenye upotevu wa pasi katika mchezo akiwa amepoteza mipira mara 27.


Kutokana na kiwango kibovu cha Tomiyasu siku ya jana inaonesha ni wazi anastahili kujilaumu kutolewa kwa timu ya taifa ya Japan katika hatua ya 16 bora kwenye michuano ya kombe la dunia.

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa