Kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta ameilaumu Arsenal kwa kupata ushindi mdogo kwenye mchezo wao wa mwisho kwenye michuano ya Europa ambapo walikuwa wakikipiga dhidi ya Zurich.
Arsenal ndio vinara wa kundi hilo wakiwa na pointi 15 baada ya kushinda mechi zao 5 na kupoteza mchezo mmoja huku wakifuatiwa na PSV mwenye pointi 13. Vijana wa Arteta wameshinda mechi 9 za nyumbani katika mashindano yote msimu huu, ukiwa ni muda mrefu zaidi kushinda mwanzoni mwa kampeni tangu 2009-10.
Bao hilo lilifungwa na Kieran Tierney katika kipindi cha kwanza cha mchezo, na mpaka kukamilika kwa dakika hizo 90 ndio bao liliipatia alama 3, huku Arteta akisema kuwa timu yake ilikuwa na makosa katika sehemu za mwisho za mchezo licha ya matokeo hayo.
Bao hilo linakuwa ni la tatu kwa mchezaji huyo kwenye Ligi ya Europa moja ambapo ni dhidi ya Celtic na kwenye ligi mabao mawili.
Beki huyo wa kushoto amelazimika kucheza nafasi ya chini kwa Tomiyasu kwa sehemu kubwa za msimu lakini alisisitiza kuwa kiwango chake cha uchezaji hakitashuka, iwe kwenye kikosi cha kwanza au la.
Kocha huyo alisema kuwa; “Siku zote tunajaribu kuanza kwa kasi zaidi. Tuna mpinzani ambaye ana jambo la kusema kwenye mchezo, tulifanya mchezo kuwa mgumu katika dakika 15, 20 zilizopita.”
Hakuishia hapo tu, alisema kuwa kuhusu kuumia kwa Tomiyasu ambaye ni mchezaji wa Kimataifa wa Japan kunawapa wasiwasi na pia hakusema kuwa atarejea muda gani, pia wikendi hii watacheza Dabi ya London dhidi ya Chelsea.