Mshambuliaji wa klabu ya timu ya taifa ya Brazil na Real Madrid Vinicius Jr ametuma salamu za pole kwa gwiji wa soka wa nchi hiyo Edison Arantes Do Nascimento maarufu kama Pele.

Mchezaji huyo ambaye aliisaidia timu ya taifa ya Brazil kupata ushindi wa mabao manne kwa moja dhidi ya Jamahuri ya Korea Kusini katika mchezo wa kombe la dunia katika hatua ya 16 bora. Vinicius Jr ametuma salamu kwa Pele baada ya ushindi huo na kumuahidi wataendelea kufanya hivo mpaka fainali ya michuano hiyo.vinicius jrGwiji Pele yupo kwenye hali mbaya kiafya ambapo anapatiwa matibabu nchini kwao Brazil katika jiji la Sao Paulo ambapo staa huyo inaelezwa yupo kwenye matibabu maalumu juu ya ugonjwa mabao unamsumbua gwiji huyo.

Vinicius Jr ameutoa ushindi walioupata dhidi ya Jamhuri ya Korea kwenda kwa gwiji Pele kama ishara ya kumkumbuka gwiji na heshima juu ya yale aliyoyafanya kwenye taifa hilo kimpira.vinicius jrBaada na kabla ya mchezo wa jana ambapo Brazil walifuzu hatua ya robo fainali wachezaji wote wa taifa hilo walibeba mabango yanayoonesha picha ya Pele kama ishara ya kutuma salamu za kumpa nguvu gwiji huyo anayepitia kipindi kigumu wakati huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa