Pablo Gavi kiungo kinda wa klabu ya Fc Barcelona amesaini mkataba mpya wa kumueka klabuni hapo mpaka mwaka 2026 baada ya mazungumzo kukamilika yaliyochukua wiki kadhaaa.

Kijana huyo atapokea mshahara zaidi aliokua akiupokea awali baada ya kusaini dili hili lipya huku hela iliyowekwa kwenye mkataba ili kumuachia kinda huyo kama ikitokea klabu ikamuhitaji ni €1B hii inaonesha ni kwa kiwango gani Barca wana mipango ya muda mrefu na mchezaji huyo mwenye umri 18.

pablo gavi

Kijana huyo ambae anasifika zaidi kwa kucheza zaidi ya nafasi moja kwenye eneo la katikati uwanjani lakini pia watu wengi wanavutiwa na aina yake ya uchezaji wake akiwa hajafunga kamba za viatu.

Kinda huyo aliejiunga na timu ya vijana ya Barcelona mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka kumi na moja alipata nafasi kwenye timu kubwa msimu wa 2021/22 baada ya kuonesha uwezo wa juu katika timu ya vijana tena akiwa na umri mdogo na kuwavutia walimu wa timu na kumpandisha timu ya wakubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa