Klabu ya Marseille ya nchini Ufaransa inatarajia kuwakaribisha Eintracht Frankfurt ya Ujerumani baada ya timu hizi mbili kupoteza mechi zao za kwanza kwenye ufunguzi wa klabu bingwa wiki iliyopita.
Marseille alipoteza akiwa ugenini dhidi ya Tottenham kwa mabao 2-0 baada ya mchezaji wao kupewa adhabu ya kadi nyekundu kitu ambacho kilipelekea Spurs kufanya mashambulizi ya hatari na kufanikiwa kupata alama tatu, huku mabao hayo yakitupiwa kimyani na Ricaharlison.
Wakati kwa upande wa Eintratch Frankfurt wao walipoteza kwa mabao 3-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Sporting CP ya Ureno huku kikiwa ni kipigo cha aibu kwa mabingwa hawa watetezi wa Europa League.
Kwahiyo hapa zinakutana timu ambazo zote zimepoteza mechi zote za kwanza kwenye ufunguzi wa klabu Bingwa hivyo hapa kila mtu atakuwa akipambana kwa hali na mali ili aweze kupata alama tatu na kujihakikishia kusonga mbele.