Rafael van der Vaart ametoa tahadhari kwa Liverpool kabla ya mpambano wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ajax kwakuwa anaamini kuwa wao si wazuri kama ambavyo wengi wanavyoamini.

Rafael:Liverpool ni wa "Kawaida Sana".

Kiungo huyo wa zamani wa Ajax aliwataja Wekundu hao kama ‘wa wastani’ kabla ya pambano lao la UCL, na kuwataja Jordan Henderson, James Milner na Joe Gomez kama ‘wachezaji wa kawaida sana’.

Rafael:Liverpool ni wa "Kawaida Sana".

Rafael Van der Vaart anaamini kuwa mashabiki wa soka wamekuwa ‘wamepofushwa’ na hali ya wastani ya timu ya Liverpool, licha ya kikosi hicho cha Jurgen Klopp kufika fainali tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya misimu mitano na kushinda Ligi Kuu.

Akiongea na kipindi cha Uholanzi Rondo, mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi alisema: “Nadhani tumepofushwa kidogo. Tunafikiri ghafla Jordan Henderson ni mchezaji HATARI. Huyo ni mchezaji wa kawaida sana”.

“James Milner pia ni mchezaji wa kawaida sana. Joe Gomez pia ni mchezaji wa kawaida sana”.

“Virgil van Dijk yuko juu, beki wa kulia na beki wa kushoto pia ni wazuri. Lakini ikiwa mambo hayaendi vizuri na washambuliaji hao hawana siku nzuri kazini, basi nadhani ni timu ya wastani sana”Alisema Rafael

Hata hivyo, Van der Vaart aliangazia tishio la wazi lililotolewa na safu nzuri ya ushambuliaji ya Jurgen Klopp, ingawa kama Mo Salah amekuwa akifanya vibaya msimu huu.

Rafael:Liverpool ni wa "Kawaida Sana".

Liverpool waliwafunga Bournemouth 9-0 Mwezi Agosti lakini wamepata ugumu wa kufunga bao.

Salah hana bao katika mechi saba za Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya Uholanzi bado italazimika kumenyana na Darwin Nunez, Roberto Firmino na Luis Diaz, ambaye amewaongoza Liverpool nyakati fulani msimu huu akiwa amefunga mabao manne.

Rafael:Liverpool ni wa "Kawaida Sana".

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa