Klabu ya Marseille inatarajia kuikaribisha klabu ya Lille hii leo katika mzunguko wao wa saba ambapo timu nyingine zikiwa zimeshacheza mechi zao za saba. Mechi za mwisho kukutana timu hizi mbili Lille alichukua alama nne.

 

Marseille Kuwakaribisha Lille

Marseiile ambayo inashirikia katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya imetoka kupoteza mchezo wao wa kwanza wakiwa ugenini dhidi ya Tottenham Hot Spurs kwa mabao mawili kwa bila huku mchezaji wao akipewa adhabu ya kadi nyekundu.

Wakati kwa upande wa Lille hashiriki mashindano ya klabu bingwa. Na mpaka sasa katika ligi Lille ameshacheza mechi sita na ameshinda mechi tatu, sare moja na kapoteza mechi mbili, Wakati kwa upande wa Marseille yeye ameshinda mechi tano huku akitoa sare moja na hajapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

 

Marseille Kuwakaribisha Lille

Marseille yupo nafasi ya tatu katika msimamo huku akiwa na alama 16, huku kwa upande wa Lille yeye akiwa na alama 10, kwahiyo tofauti ya alama hapo ni sita kati ya timu hizi mbili.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa