Kylian Mbappe ameshindwa kuchagua ni mchezaji gani kati ya Messi na Ronaldo anahisi ni bora zaidi ya mwenzake.
Fowadi huyo wa Ufaransa alikua akimwabudu Ronaldo, lakini sasa anashirikiana na Messi katika klabu ya PSG, hivyo usimfanye achague kati ya hao wawili.
“Nampendelea nani? Ni sawa na kuchagua kati ya baba yako au mama yako, huwezi,” Mbappe alisema.
“Kwa wale wote wa kizazi changu, Ballon d’Or bila shaka inahusishwa na vita kati ya Messi na Cristiano. Nikichimba sana kwenye kumbukumbu yangu, pia namkumbuka kidogo Ronaldinho (mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2005).
“Lakini, kusema ukweli, kila kitu kimekandamizwa na wale wawili wenye tamaa! Wameshiriki tuzo kwa muda mrefu sana. Kila mwaka, kama kila mtu mwingine, nilijiuliza ni yupi kati yao angepata. Nikiangalia nyuma, vita hivyo vilikuwa hatari sana.”
Tuzo kumi na mbili za Ballon d’Or, takriban mabao 1500 ya klabu na msururu kamili wa vikombe kati yao. Kuchagua kati ya Messi na Ronaldo si kazi rahisi.
Bado, umeona maoni ya baadhi ya wachezaji bora duniani wa zamani na wa sasa, kwa hiyo wewe unamchagua nani?