Nyota wa klabu ya Paris Saint Germain Kylian Mbappe ameweka wazi kuwa rais wa nchini Ufaransa Emmanuel Macron alimwambia abaki PSG kuliko kuhamia klabu ya Real Madrid kwenye majira haya ya kiangazi.

Mbappe mwenye miaka 23 alikuwa karibu kujiunga na klabu ya nchini Hispania Real Madrid kwa uhamisho huru, kabla ya kubadilisha mawazo yake dakika za mwisho mwezi May na kusaini kandarasi ya miaka mitatu kusalia kwenye klabu ya ya PSG.

Mbappe, Mbappe: Rais Emmanuel Macron Aliniambia Niikatae Real Madrid, Meridianbet

“Sikuwai kufikilia nitaongea na rais Macron kuhusu hatma ya karia yangu,” Mbappe alilimbia New York Times. “Nikitu kinachopagawisha, kiukweli kinatia uchizi.”

“Aliniambia, nataka ubaki,” Mbappe alisema. “Sitaki uondoke sasa. Wewe ni muhimu sana kwenye nchi. Bila shaka rais anaposema hivyo kwako inakuwa na maana.”

Awali Kylian alisema ilikuwa na Mradi wa PSG wa michezo na sio pesa, vitu au mambo mengine ambayo yalimpekea kufanya maamuzi yake.

“Popote nitakapokwenda  nitapata pesa, mimi ni mchezaji wa aina hiyo popote nitakapokwenda.”              Alisema Mbappe

Mbappe mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Ufaransa ameshafunga magoli saba, kwenye michezo mitano aliyocheza mpaka sasa msimu huu, huku pia leo akitarijiwa kuwepo kwenye kikosi cha PSG ambacho kinamkaribisha Juventus kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya.

Lakini pia Kylian hakuweza kuondoa uwezekano wa yeye siku moja kucheza kwenye klabu ya Real Madrid huko mbeleni: “Huwezi jua nini kinakwenda kutokea, hujawai kuwa kule {Madrid} lakini inaonekana kama ni nyumbani kwaki  au kitu kama hicho.”


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa