Mbappe nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa amefunguka kwa kinachoendelea kati yake na mchezaji mwenzake Neymar Jr.
Kumekua na taarifa mbalimbali siku kadhaa nyuma kua wachezaji hao hawapikiki kwenye chungu kimoja na hali hiyo ilitokana na Klian Mbappe kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya PSG na mkataba huo unaelezwa ulimpa nguvu mchezaji huyo ndani na nje ya uwanja na inaelezwa Mbappe alihitaji Neymar auzwe klabuni hapo jambo lililochochea ugomvi huo.
Mbappe amefunguka kua yeye na Neymar wana uhusiano mzuri na wanaheshimiana lakini inategemea na wakati kuna muda wanakua marafiki sana na kuna muda wanakua kawaida lakini kikubwa anasema heshima ipo baina yao.
Pamoja na maneno yanayoendelea baiana ya wachezaji hao wawili lakini wanaendelea kushirikiana vizuri uwanjani na kuisaidia klabu hiyo kupata matokeo.

