KLABU ya Geita Gold FC imewasili nchini Sudan kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Hilal Alsahiri utakaochezwa kesho Jumapili.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu wa Geita Gold, Felix Minziro inaipeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga za kimataifa.

Mshambuliaji wa timu hiyo George Mpole alipata maumivu kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya msafara kuelekea nchini Sudan hivyo atakosekana kwenye mchezo huo.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Khartoum kabla ya ule wa marudio ambao unatarajiwa kuchezwa Septemba 17,2022 Uwanja wa Mkapa.

Jana mchana, Septemba 9,2022 Geita waliwasili Sudan na wameanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa