Klabu ya Tottenham Hotspur imethibitisha kufanikisha usajiri wa mchezaji kutoka klabu ya Udinese ya Italia Destiny Udogie kwa ada yauhamisho  wa kiasi cha €18milioni huku kukiwa na kipengere cha pesa kuongezeka kaisi cha  €7milioni.

Destiny Udogie kwasasa yupo jijini London kwa ajiri ya kukamilisha vipimo vya afya. Mchezaji huyo wakimataifa wa Italia, usiku wa jana hakuwepo kwenye kikosi kilichofunngwa na klabu ya Milan 4-2 ili kuafanikisha uhamisho wake huo.

Tottenham, Tottenham Kukamilisha Usajiri wa Udogie, Meridianbet

“Nina furaha sana. Nina shauku kubwa ya kwenda kucheza Premier League, kufanya kazi na Conte na kusajiriwa na klabu ya Tottenham.

“Nimeshawishika kwamba naweza kujiboresha zaidi nikiwa chini ya Conte, kwa sasa, ni muhimu kurudi Udinese kwa mkopo, kama ninataka kuwa na msimu mzuri.” Alisema Udogie.

Destiny Udogie anamiaka 19 na ni mchezaji wa kimataifa wa Italia, huku akiichezea timu ya taifa ya Italia ya vijana chini ya miaka 21. Wakati wazazi wakiwa na asili ya Nigeria.

Kwenye safari yake ya kwenda London alisindikizwa na msimamizi wake Gianluca Di Carlo, mawakala wake Stefano Antonelli na Ferdinando Guarino.

Pia japo klabu ya Tottenha imesajiri mchezaji huyo kwa uhamisho wenye thamani ya €18milioni, lakini watamuacha kwa mkopo kwenye klabu hiyo kwa mkopo wa muda mrefu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa