Beki wa Arsenal William Saliba ametua Ufaransa kuelekea Marseille ambako amesajiliwa na klabu hiyo kwa mkopo.

The Gunners walikuwa kwenye mazungumzo na klabu hiyo ya Ligue 1 kwa wiki kadhaa kuhusu dili ya mkopo wa mchezaji huyo wa miaka 21 ambaye alitumia nusu ya msimu na klabu ya Nice kwa mkopo.
Na makubaliano sasa yamefikiwa na mlinzii huyo amepewa ruhusa ya kwenda Ufaransa kukamilisha uhamisho wake huko The Stade Velodrome.
Saliba alitua Ufaransa siku ya Jumanne asubuhi kwaajili ya kufanyiwa vipimo na kukamilisha usajili wake na Marseille.
Hii itakuwa mara ya tatu kuondoka kwa mkopo tangu atue Emirates mwaka 2019 kwa dau la £27m ($37m) akitumie misimu na Saint-Etienne na Nice.

Arsenal wanadai bado wanamipango na beki huyo licha kutolewa kwa mkopo na watamuangalia tena mwisho wan msimu 2021-22.
Arsenal sasa wanaendelea na mipango yao ya kutaka kuinasa saini ya beki wa kati wa Brighton Ben White dili ambayo inasemekana inaweza kufika £50m.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!


