Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi kurudia kile walichokifanya mwaka 2014 kumzuia staa wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi.

Uholanzi ambao wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuifunga timu ya taifa ya Marekani kwa mabao matatu kwa moja.Uholanzi watakutana na timu ya taifa ya Argentina katika mchezo wa robo fainali siku ya ijumaaa.van gaalMwaka 2014 Uholanzi walikutana na Argentina katika nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Brazil na Uholanzi wakitolewa kwenye mikwaju ya penati. Kocha Van Gaal anaamini vijana wake wanatakiwa kufanya juhudi wakati huu kama 2014 ili kumfanya Messi kutokua na madhara kama 2014.

“Messi ndio mchezaji muhimu zaidi na mbunifu zaidi kwenye timu yao. Hawa ndio ndio wachezaji mhimu kila wakati. Miaka nane iliyopita tulifanikiwa kwenye kombe la dunia nchini Brazil, Tulifanikiwa kumzuia Messi . Hakupiga mpira wakati ule.van gaalKocha Van Gaal anaamini walikua bora sana wakati ule lakini bahati mbaya walipoteza kwenye mikwaju ya penati, Lakini wito kwa wachezaji wake wasasa ni kuiga kile kilichofanywa kwa wakati ule ili kumzuia Messi ambae ndio mchezaji tishio zaidi kwa upande wa Argentina.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa