Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia anayekipiga kwa wekundu wa msimbazi klabu ya Simba Moses Phiri amezungumza kuhusu wachezaji wenzake klabuni hapo.

Mshambuliaji huyo ambaye ameweka rekodi ya kua mchezaji wa kwanza kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguko wa kwanza na kufunga mabao 10. Moses Phiri mpaka sasa amekaa kileleni kwenye orodha ya wafungaji bora akiwa sambasamba na mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele.moses phiriPhiri anaeleza klabu ya Simba ina wachezaji wazuri ambao anaweza kushirikiana nao kwenye duru la pili na kufunga mabao mengi zaidi ya haya kwenye ligi kuu ya NBC pamoja na ligi ya mabingwa Afrika.

Moses Phiri amekua na wastani mzuri wa kupachika mabao tangu atue klabuni hapo kwenye ligi kuu ya NBC pamoja na ligi ya mabingwa Afrika ambapo alifanikiwa kufunga takribani mabao manne kwenye michez ya kufuzu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa