Moses Phiri Anakimbiza Mwizi Kimya Kimya

Mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Moses Phiri ameendelea kumkimbiza mwizi kimya kimya katika mbio za kuwania ufungaji bora wa ligi kuu NBC Tanzania bara.

Mshambuliaji huyo leo ameweza kuingia kambani mara mbili katika mchezo wa ligi kuu ya NBC baada ya klabu yake ya Simba kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo uliopigwa katika dimba la Ushirika mkoani Kilimanjaro.

Moses Phiri leo ameweza kufikisha magoli nane baada ya kufunga mara mbili leo dhidi ya Polisi Tanzania hivo kubakisha magoli mawili kumfikia nyota wa klabu ya Yanga Fiston Mayele ambae ndio kinara akiwa anaongoza akiwa na magoli 10 mpaka sasa.Fiston Mayele ambao alikaa takribani miezi miwili bila kufunga bao katika mchezo wa ligi kuu ya NBC lakini ameweza kuja kuwapiku washambuliaji wengine kwa kufunga mabao saba katika michezo mitatu ya hivi karibuni na kukaa kileleni kwa jumla ya mabao 10.

Moses Phiri na Fiston Mayele ndio washambuliaji wanaoonekana kuweza kuchuana kwenye mbio za ufungaji bora kutokana na ubora wao pamoja na klabu wanazozitumikia kuonekana kutengeneza nafasi mara kwa mara na kuwasaidia wao kufunga.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.