MSHAMBULIAJI wa Simba, Moses Phiri ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki ndani ya mwezi Septemba.

Ni mashabiki ambao walikuwa wanachagua kwa kupiga kura kupitia mitandao ya kijamii ambapo ni Phiri alikuwa ameingia fainali na Mzamiru Yassin pamoja na Clatous Chama kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa tuzo hiyo kwa mwezi Septemba inakwenda kwa Phiri. Ikumbukwe kwamba mwezi Agosti ilikwenda kwa Chama ambaye aliwashinda Sadio Kanoute na Pape Sakho.

Phiri amebebwa na ubora wake ambao ameonyesha kwenye mechi za hivi karibuni.

Akifunga mabao manne kwenye ligi kuu na mabao manne kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Huku akiwa amesaidia kwa asilimia 100 ushindi wa Simba kwenye mechi hizo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa