Afisa habari na mawsiliano wa klabu ya Simba wekundu wa msimbazi Ahmed Ally amefunguka kuhusiana na usajili ambao klabu hiyo utaufanya kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Ahmed Ally amethibitihsa kua klabu ya Simba haitafanya usajili wowowte kabla haijapokea mapendekezo kutoka kwa kocha wa timu hiyo Juma Mgunda. Afisa habari huyo amesema Simba itafanya usajili kwa kuzingatia kocha mahitaji ya kocha aliyowapatia viongozi wa timu hiyo.ahmed allyWekundu wa Msimbazi wana mpango wa kuingia sokoni kwenye dirisha dogo kwa kishindo sana kama ambavyo alieleza mkurugenzi wa klabu hiyo Barbara Gonzalez mara ya mwisho akizungumzia usajili. Lakini wekundu wa msimbazi hawataki kuingia sokoni bila kusikiliza wapi ambapo kocha ameona mapungufu ndipo viongozi waingie sokoni.

Ahmed Ally ameliweka suala hilo wazi na kueleza kua sokoni Januari lazima klabu hiyo iingie kwakua wanaona wanapaswa kufanya hivo lakini lazima wapitie kuchukua mapendekezo ya kocha Juma mgunda.ahmed allyMpaka sasa klabu ya Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama zake 34 huku wakiwa nyuma ya vinara na mabingwa watetezi klabu ya Yanga na nafasi ya pili inayoshikiliwa na klabu ya Azam Fc.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa