Gabriel Jesus Afanyiwa Upasuaji wa Goti

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Brazil Gabriel Jesus anaripotiwa kufanyiwa upasuaji wa goti lake siku ya leo baada ya kuumia siku kadhaa akiitumikia timu ya taifa ya Brazil.

Mshambuliaji huyo ambaye alipata majeraha katika mchezo wa mwisho wa kundi G ambapo timu ya taifa ya Brazil ilimenyana na timu ya taifa ya Cameroon na kupoteza kwa bao moja kwa bila huku mshambuliaji huyo akipata majeraha.Gabriel JesusGabriel Jese amefanyiwa upasuaji wa goti lake leo na upasuaji umeenda vizuri na tayari ameanza matibabu ya ukarabati wa afya yake punde yu baada ya upasuaji wake kufanikiwa kama taarifa zinavyoeleza.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Arsenal alipopata majeraha aliondolewa kwenye kikosi cha Brazil na kutarajiwa kukaa nje kwa wiki kadhaa lakini majeraha yameonekana kua makubwa kuliko ilivyotarajiwa, N a kwasasa staa huyo atakaa nje kwa miezi kadhaa kutokana na upasuaji aliofanyiwa.Gabriel JesusGabriel Jesus ambaye amekua na msimu mzuri pamoja na klabu yake ya Arsenal lakini kwasasa atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa jambo ambalo ni pigo kubwa sana kwa klabu yake ya Arsenal.

Acha ujumbe