Xabi Alonso Kumrithi Ancelotti

Kocha wasasa wa klabu ya Bayern Leverkusen Xabi Alonso ambaye amewahi kuvitumikia vilabu vya Liverpool, Real Madrid, na Bayern Munich anatarajiwa kuchukua mikoba ya kocha Carlo Ancelotti.

Kocha Carlo Ancelotti amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu ya Real Madrid na anatarajiwa kujiunga na timu ya taifa ya Brazil kama vyanzo vinavyoeleza, Huku Xabi Alonso akitajwa zaidi kuchukua mikoba yake.Xabi alonsoKocha huyo wa klabu ya Bayern Leverkusen vyanzo mbalimbali ndani ya Real Madrid vinaeleza anaongoza orodha ya makocha ambao wanatarajiwa kumrithi Carlo pale ambapo mkataba wake utakapokua umememalizika ndani ya klabu hiyo.

Xabi Alonso amekua kwenye msimu mzuri ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen ambapo aliisaidia timu hiyo kukaa kwenye nafasi za juu kabla ya hapo ilikua kwenye nafasi za chini vilevile akiipeleka nusu fainali ya Uefa Europa League.Xabi alonsoGwiji huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool anaonekana kuiva ambapo ameshafundisha timu za vijana za klabu ya Real Madrid na sasa anaifundisha Bayern Leverkusen na ndio sababu ya Real Madrid wanaona anafaa kuvaa viatu vya Carlo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.