Kocha wa Ghana Otto Addo kila mara alitarajia kuwa mchezaji wa Spurs Son Heung-min angeendelea kuwa na taaluma nzuri, huku akisifu tabia na nidhamu ya nahodha huyo wa Korea Kusini.

Korea itamenyana na Ghana katika mechi ya pili ya Kundi H Kombe la Dunia hapo kesho wakati Korea ilitoka sare ya 0-0 na Uruguay, katika mchezo ambao ulikuwa mgumu baada ya kupiga shuti moja pekee lililolenga lango, Ghana ilipoteza kwa mabao 3-2 kutoka kwa Ureno.
Son alipona jeraha la jicho ili kushiriki katika mechi ya ufunguzi ya Korea huko Qatar, ingawa mshambuliaji huyo wa Tottenham alilazimika kuvaa barakoa ya kumlinda usoni kwake.
Naye Addo, ambaye alifanya kazi na Son wakati alipokuwa kocha wa timu ya vijana ya Hamburg kati ya 2009 na 2015, alisema alitambua uwezo wa mshambuliaji huyo mapema, na atajaribu kumzuia kila mshambuliaji.

Addo amesisitiza kuwa walifanya vyema dhidi ya Ureno, na Son ni mchezaji mzuri sana, anafanya kazi kati ya safu na anapiga mashuti mazuri sana. Kocha huyo alikuwa na furaha kuwa naye alipokuwa kocha wa vijana chini ya miaka 19 huko Hamburg.
Aliendelea kumsifia Son na kusema kuwa ana tabia nzuri sana ni mchapakazi na anapenda sana tabia yake, nidhamu aliyonayo na amekuwa mzuri sana kwasababu alifanya nae kazi.

Kupoteza mechi yao ya kwanza katika Uwanja wa Education City kunaweza kuifanya Ghana kuondoka mapema, ingawa ushindi unaweza kuwainua hadi nafasi ya pili kwenye kundi mwishoni mwa siku, kulingana na matokeo ya Ureno kukutana na Uruguay.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


