Cameroon Ndio Taifa La Kwanza Kuifunga Brazil Fainali za WC

Timu ya Taifa ya Cameroon imekuwa taifa la kwanza kuifunga Brazil katika fainali hizi za Kombe la Dunia ambapo hapo jana wamepachikwa bao 1-0 katika mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi.

 

Cameroon Ndio Taifa La Kwanza Kuifunga Brazil Fainali za WC

Bao hilo lilifungwa na Vicent Aboubakar katika dakika ya 90+2 na bao hilo hilo likasababisha mchezaji huyo kupata kadi ya pili ya njano, ambayo ikageuka kuwa nyekundu kwa kosa la kuvua jezi kwa kushangilia bao hilo kwani alishapewa kadi ya njano mwanzo.

Lakini licha ya kufunga bao hilo na kupata pointi tatu muhimu, Taifa la Cameroon limeshindwa kufuzu hatua ya 16 bora kutokana na Taifa la Uswizi kushinda mechi yao kwa mabao 3-2 dhidi ya Serbia hapo jana na kupata pointi 6.

Cameroon Ndio Taifa La Kwanza Kuifunga Brazil Fainali za WC

 

Kwahiyo sasa kwenye Kundi G ambae ameenda katika hatua ya 16 bora ni Brazil pamoja na Uswiz ambao wote wana pointi sita, halafu Cameroon na Sebia wao safari yao imeishia hapa hapa wanarudi nyumbani kujipanga upya.

Hatua ya 16 bora Brazil atacheza dhidi ya Korea Kusini, wakati Uswizi itacheza dhidi ya Ureno ili kutinga robo fainali.

Cameroon Ndio Taifa La Kwanza Kuifunga Brazil Fainali za WC

 

 

Acha ujumbe