Ligi kuu ya NBC ya msimu huu imekua kwenye ushindani mkubwa kuanzia kwenye timu mpaka wachezaji ambao wanachuana kwelikweli kuhakikisha timu zao zinafanya vizuri.

Msimu huu ukiacha vita ya kugombea kiatu cha dhahabu mwisho wa msimu kwa washambuliaji ambao watakua wamefunga mabao matatu, Lakini vita nyingine msimu huu ni kwa wataalamu wakupiga pasi za mwisho ambapo mpaka sasa wanachuana kwelikweli.

Mpaka sasa wanaoongoza kwa kupiga pasi za mabao wapo watatu huku kila mmoja akiwa na pasi sita za mabao ambapo wapo waatu ambao ni Clatous Chama kutoka Simba, Ayoub Lyanga kutoka Azam Fc, pamoja Sixrus Sabilo kutoka Mbeya City ya mkoani Mbeya.pasiWengine ambao wanachuana kwenye upigaji wa pasi za mwisho kwenye NBC msimu huu ni Saidoo Ntibazonkiza kutoka Geita Gold mwenye pasi tano akifuatiwa na Mohamed Hussein kutoka Simbamwenye pasi tano za mabao.

Msimu huu kwenye ligi kuu ya NBC inaonesha namna ushindani umeongezeka maradufu kwasababu imezoeleka ushindani mara nyingi unakua kwenye kiatu cha ufungaji ila msimu huu hadi kwenye pasi za mwisho ushindani umeongezeka.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa