Mkurugenzi wa klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A ameeleza hawana mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Morocco Sofyan Amrabat aliyepo klabuni hapo.

Kiungo huyo ambaye ameonesha ubora mkubwa kwenye michuano ya kombe la dunia huku akiisaidia timu yake ya taifa ya Morocco kuongoza kundi F mbele ya vigogo kama Ubelgiji na timu ya taifa ya Croatia wakiwa na alama zao saba.amrabatKiungo Sofyan Amrabat amekua akihihusishwa na klabu ya Tottenham ya nchini Uingereza chini ya mwalimu Antonio Conte lakini mkurugenzi wa Fiorentina alipoulizwa kuhusu kiungo huyo kuelekea Spurs Jnauari alikanusha kwa kusema “Hatuna mpango wa kumuuza. Tuna nafasi ya kumuongezea mkataba, Hatuna haja ya kuharakisha kwasababu ypo kwenye mipango yetu.

Kiungo huyo fundi wa mpira kwasasa amekua akihusishwa na vilabu vikubwa na hiyo ni kutokana na ubora mkubwa aliouonesha kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar akiwa kama sehemu ya mhimili wa timu hiyo.amrabatMkurugenzi wa klabu ya Fiorentina amesisitiza Amrabat hatauzwa mwezi Januari kwasababu yupo kwenye mipango ya klabu yao kwasasa hivo watahakikisha kiungo huyo anasalia klabuni hapo kwa muda zaidi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa