Simba Huko Misri Wanazichapa Pasi ni Balaa!

SIMBA chini ya kocha,Zoran Maki ni mwendo wa kugusa na kuachia tu na wala hataki mambo mengi na hiyo ni kwaajili ya kuhakikisha anakiandaa kikosi hiko vyema kuelekea msimu ujao katika michuano mbalimbali ambayo timu hiyo watashiriki.

Simba kwa sasa wapo nchini Misri wakiwa katika maandalizi ya msimu mpya chini ya kocha huyo ambapo kibarua chake cha kwanza kitakuwa katika mchezo wa fainali ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga.

Taarifa kutoka katika kambi hiyo imelitaarifu Championi Ijumaa kuwa katika mazoezi hayo yanayoendelea hatki kuona mchezaji akigusa mpira zaidi ya mara mbili kabla hajauachia ikiwa ni kuwazoesha wachezaji kuachia mpira na kucheza kwa haraka zaidi.

“Kocha Maki hataki kuona wachezaji wakikaa na mpira kwa muda mrefu bila kuachia,anahitaji kuona wachezaji wakipiga pasi za haraka haraka ili kuzoea ikiwa ni miongoni mwa falasafa yake,tayari wachezaji wameanza kuonyesha kukubaliana na mazingira mapya.


“Wachezaji wanayofuraha ya kutosha mazoezini chini ya utawala wa kocha mpya na hii inaonyesha ni kwa jinsi gani kuna kitu wataenda kukifanya msimu ujao,mazoezi yanaendelea kuhakikisha kuwa timu inakuwa kamili kwaajili ya msimu mpya,”kilisema chanzo hiko.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmedy Ally amesema kuwa “Kwasasa maandalizi yetu yanakwenda vizuri huku tukiwa na lengo la maandalizi mazuri ya wiki ya Simba Day,wachezaji wanafuraha na kocha anafanya kazi yake kuhakikisha Simba inakuwa timu tishio.

Acha ujumbe