Mashabiki wa klabu ya Atletico Madrid wameanzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kushinikiza klabu yao kutokumsajiri mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 37, mwishoni mwa mwezi June, aliwasilisha ombi la kutaka kuaondoka kwenye klabu ya Man Utd licha kubakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Madrid, Madrid: Mashabiki Waanzisha Kampeni ya Kumpinga Ronaldo, Meridianbet

Awali, klabu za Chelsea na FC Bayern ziliripotiwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo kabla kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho.

Taarifa kutola nchini Hispania zinasema kuwa klabu ya Atletico Madrid inahitaji huduma ya mshambuluaji huyo na wako tayari kumuweka sokoni Antoine Griezmann ili kuweza kupunguza bill ya mshahara kwa ajiri kufanikisha usajiri wa Ronaldo.

Mashabiki wa Atletico Madrid hawataki klabu yao imsaini mchezaji huyo, ambaye alikuwa mchezaji wa wapinzani wao Real Madrid. Mashabiki wameanzisha kampeni ambayo wameipa jina  ‘#ContraCR7’ ikiwa na maana ya kumkataa mchezaji huyo.

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa