Nyota wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo yuko tayari kupunguza mshahara wake ili kuweza kurahisisha njia yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Atletico Madrid.

Ronaldo alishaweka wazi nia ya kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu,  kulingana na Ben Jacobs ili aweze kurahisha usajiri huo mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ureno yuko radhi kupunguza kwa asilimia 30 ili ajiunge na Atletico Madrid.

Ronaldo, Ronaldo Kupunguza Mshahara Wake Ili Kujiunga na Madrid, Meridianbet

Licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kuwa tayari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 30, lakini bado timu itakayohitaji huduma yake itapaswa kulipa takribani £300,000 kama mshahara wake.

Awali kulikuwa na tetesi kuwa Chelsea, PSG na Bayern Munich zilikuwa zinahitaji huduma yake kabla ya vilabu hivyo kukanusha  na sasa ni ATL Madrid pekee ambayo imebakia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Ronaldo pia alishawai kuichezea timu ya Real Madrid ambao ni wapinzani wakubwa wa ATL Madrid ambapo alitumikia kuanzia mwaka 2009 hadi 2018 na kufanikiwa kufunga magoli 450 kwenye michezo 438.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa