Klabu ya Barcelona imefanikiwa kukamilisha uhamisho wa umiliki wa hati za matangazo ya runinga kwa kampuni kutoka nchini Marekani ya Sixth Street kwa miaka 25 ambapo klabu hiyo inatarajia kupata kiasi cha €400milioni kwenye asillimia 15 za hisa hizo.

Awali klabu ya Barcelona mwezi June walifanikiwa kuuza kwa mara ya kwanza asilimia 10 ya hati milikia za matangazo ya runingwa kwa kampuni hiyo na kufanikiwa kupata kiasi cha €267milion.

Mpaka sasa klabu ya Barca imeshafanikiwa kuuza hati miliki za matangazo mara mbili kwa kampuni moja, na sasa wako kwenye mpango wa kuhakikisha wanafanikiwa kupata kiasi €100milion kwenye hati za matangzo kwenye mauzo ya mara tatu.


Ufanikishaji wa mauzo ya hati hizo imeisaidia klabu ya Barcelona kuweza kupunguza deni kwa kiasi kinachokadiriwa kufikia €550milion na kusaidia klabu hiyo kuweza kupata kibali cha kutumia kila pesa inayongia.

Ili kuweza kupata pesa zaidi klabu ya Barcelona iko tayari kuuza umiliki wa asilimia kadhaa kwenye studio yao, ambapo inasidikia kuwa hazitazidi aslimia 49, huku studio hiyo ikiwa imeteka soko la ukanda huo kwa asilimia 20.

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa