HATIMAYE beki wa kati wa Al Hilal ya nchini Sudan, Mohammed Outtara aaga rasmi katika klabu yake hiyo huku akitajwa mbioni kujiunga Simba ambayo imekamilisha usajili wa beki huyo mwenye uraia wa Burkinafaso.

Outtara mwenye umri wa miaka 29 ni moja kati ya mabeki bora akiwa amewahi kukipiga ndani ya Wyda Casablanca ya Morroco anatajwa kuja kuziba pengo la Pascal Wawa ambaye tayari amechwa na Simba.

Chanzo cha ndani kutoka Simba kilisema kuwa mchezaji huyo atayari ameshakamilisha kila kitu na baada ya kuaga kwao atasafiri moja kwa moja kutoka Sudan na kwenda Misri kwaajili ya utambulisho utakaofanyika huko huko na kuanza mazoezi na wenzake.

“Outtara tayari ameshaaga kwao nchini Sudan katika klabu yake ya Al Hilal na hivi karibuni anatarajiwa kuingia huku nchini Misri ambapo atafanyiwa utambulisho kama ilivyokuwa utaratibu wa timu kisha ataanza mazoezi na wenzake,”kilisema chanzo hiko.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa