Cristiano Ronaldo Akataa Mshahara wa £250milioni

Mchezaji nyota wa kimataifa kutoka nchini Ureno anayekipiga kwenye klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo amekataa mshahara wa £250milioni kutoka kwenye klabu inayoshiriki ligi kuu ya nchini Saudi Arabia.

Klabu ambayo ilikuwa inahitaji huduma ya Cristiano Ronaldo ilishaanda mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya £250milion, huku klabu ya Man Utd ikipata kiasi cha £25milioni kama ada ya uhamisho. Mpaka sasa klabu ambayo ilikuwa inahitaji huduma ya Ronaldo, bado haijawekwa wazi zaidi ya kupatikana taarifa kuwa inatokea nchini Saudi Arabia.

Cristiano Ronaldo

Ikiwa Ronaldo angekubali uhamisho basi angekuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani, lakini Mchezaji huyo mwenye miaka 37 bado anashauku ya kutaka kuendelea kucheza barani ulaya hasa mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Cristiano Ronaldo alishaweka wazi kwa klabu na kocha Ten Hag kuwa anahitaji kuondoka kwenye klabu hiyo katika dirisha la usajiri hili la majira ya kiangazi.

Ronaldo mpaka sasa hajaweza kujumuika na kikosi cha Man Utd kwenye safari na michezo ya pre-season kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini amekuwa akifanya mazoezi binafsi ili kujiandaa na msimu mpya utakao anza mwezi August.

 

Acha ujumbe