KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen ametaja sababu za kuwaita nyota 24 katika kikosi chake.

Stars wamebakiwa na hatua tatu kwa ajili ya kufika fainali ya michuano hiyo ambapo michuano hiyo ni ya mtoano.

Kim, Kim Ataja Sababu za Kuwaita Nyota 24, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi hayo Kim amesema kuwa “Timu inaingia kambini leo Ijumaa (jana) kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ya kufuzu michuano ya CHAN.

“Mazoezi yataanza kesho jumamosi na mchezo wa kwanza tutacheza Julai 23 mwaka huu huku ule wa marudiano utakuwa Julai 30, mechi zote zinachezwa uwanja wa Mkapa.

“Vigezo vilivyotumika kwa kuwachukua wachezaji ni viwango vyao walivyoonyesha katika michezo waliyocheza wakiwa na klabu zako. Tutakuwa na muda mzuri na mwingi wa kufanya maandalizi.”

Stars Ina nafasi ya kuvuka katika hatua inayofuatia kutokana na aina ya timu ambazo wanakutana nazo hivyo kikubwa kinachohitajika ni juhudi za wachezaji kufuata maelekezo ya kocha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa