HASSAN Kessy beki wa zamani wa Yanga na Simba ambaye msimu wa 2021/22 alikuwa ni mali ya KMC anatajwa kumalizana na mabosi wa Ruvu Shooting.

Kessy atajiunga na Ruvu Shooting akiwa ni mchezaji huru baada ya KMC kuweza kumshukuru kwa mchango wake ambao aliweza kuutoa kwa msimu uliopita.

Ofisa Habari wa KMC,Christina Mwagala amesema kuwa Kessy wao wameshamalizana naye labda kwa wahusika wenyewe.

“Kuhusu Kessy,(Hassan) sisi tumeshamalizana naye tayari sijui labda kwa huko,” Julai 20,KMC walimuaga rasmi beki huyo.
Kwa upande wa Ruvu Shooting,Ofisa Habari Masau Bwire alisema kuwa mipango ikiwa tayari kila kitu kitawekwa wazi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa