Mshambuliaji wa Tottenham Spurs Harry Kane anaamini kuwa Uingereza hawana hofu tena ya kukiri kuwa wanaweza kushinda Kombe la Dunia, ambapo anafikiri kuwa kiwango kibovu cha Three Lions kinaweza kuwa faida kwao.

 

Kane: Hatuogopi Tena Kusema Tunaweza Kushinda Kombe la Dunia

Kane na wenzake wanaelekea Qatar kwa Kombe la Dunia la 2022 wakiwa wamepungukiwa na kiwango baada ya kushushwa ngazi ya juu ya Ligi ya Mataifa kufuatia sare tatu na kupoteza tatu katika Kundi A3.

Kikosi cha Southgate hakijashinda tangu ushindi wa 3-0 wa kirafiki dhidi ya Ivory Coast mwezi Machi lakini nahodha Kane anasema Three Lions hawatakwepa kueleza matumaini yao ya kubeba Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo aliiambia Sky Sports kuwa; “Lazima tuamini kuwa tunaweza kushinda, ninaangalia nyuma Uingereza miaka 10, 15 iliyopita na ilikuwa karibu kama tuliogopa kusema tunataka kushinda.”

Kane: Hatuogopi Tena Kusema Tunaweza Kushinda Kombe la Dunia

Mchezaji huyo alisema kuwa anadhani moja ya mabadiliko makubwa ambayo wamefanya kwa miaka minne au mitano iliyopita na Gareth sio kuogopa kusema hivyo, na itakuwa ngumu na wanalazimika kufanya kazi kwa bidii sana, kuwa na bahati kidogo na kuwa na mambo mengi yatakayowasaidia kufikia hilo.

Presha imeongezeka kwa Southgate baada ya matokeo mabaya ya Ligi ya Mataifa, lakini Kane anasema kutokuwa na ushindi kumepunguza matarajio na huenda ikasaidia Uingereza katika mechi yao ya kwanza ya Novemba 21 dhidi ya Iran.

“Mchezo wa kwanza ni muhimu sana, kwa hakika, bila shaka hakijakuwa kipindi kizuri zaidi kwa muda mrefu kwa Uingereza tangu Gareth achukue jukumu la kuinoa timu hiyo hatujapata maajabu  kama tulivyokuwa.”

Kane: Hatuogopi Tena Kusema Tunaweza Kushinda Kombe la Dunia

Hakuishia hapo aliongeza kwa kusema kuwa anahisi kuwa wangeshinda kila mchezo kabla ya mashindano hayo ingekuwa wana uhakika wa kushinda na watashinda, na hiyo inaweza kuja na shinikizo tofauti.

Kuhusu utimamu wa Kane, ambaye amekuwa akiichezea Tottenham kila mara katika Ligi ya Primia, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anaamini kuwa michuano hiyo ya katikati ya msimu itamsaidia kupiga hatua.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa