Aleksandar Mitrovic amerejea mazoezini na Serbia na yupo nje ya  maumivu baada ya jeraha lake la mguu, huku nchi yake ikiwa na kibarua kizito cha kukabiliana na Brazil kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwenye mechi yao ya kwanza.

 

Mitrovic Arejea Mazoezini Kuwakabili Brazil

Mitrovic alifunga bao lililoipeleka Serbia kwenye Kombe la Dunia, akifunga kwa kichwa dakika ya 90 dhidi ya Ureno mnamo Novemba 2021 na kutinga kileleni katika kundi lao la kufuzu na nafasi ya moja kwa moja nchini Qatar.

Lakini Mitrovic, ambaye amefunga mabao 50 katika mechi 76 alizoichezea nchi yake, alikosa mchezo wa mwisho wa Fulham kabla ya kujiunga na Serbia kutokana na tatizo la mguu.

Kocha mkuu wa Serbia Dragan Stojkovic hapo awali alitania Mitrovic atakwenda Kombe la Dunia “bila mguu”, na alikuwa na taarifa chanya juu ya utimamu wa mshambuliaji huyo kabla ya mechi yao ya kwanza akiwa na Brazil wanaopendelewa kabla ya michuano hiyo katika Kundi G.

Mitrovic Arejea Mazoezini Kuwakabili Brazil

Stojkovic amesema kuwa; “Mitrovic amekuwa akifanya kazi na timu, ametoka katika maumivu pale alipojeruhiwa, hiyo ni habari njema.”

Lakini kocha huyo almekuwa na matumaini zaidi juu ya kupatikana kwa mchezaji wa Juventus Filip Kostic akisema kuwa ana shida ya misuli na ana shaka juu yake. Serbia itamenyana Brazil hii leo wakitafuta pointi tatu.

Mitrovic Arejea Mazoezini Kuwakabili Brazil

Lakini Mitrovic anaweza kuanza au akae benchi huku akitazamiwa kama mchezaji muhimu kwa Taifa hilo hii leo.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa