Mchezaji wa PSG na timu ya Taifa ya Brazil Neymar amesema kuwa  hana uhakika kama atapata fursa ya kuiwakilisha Brazil kwenye Kombe lingine la Dunia baada ya mashindano ya mwaka huu nchini Qatar.

 

Neymar: "Qatar Inaweza Kuwa Kombe Langu La Mwisho"

Mchezaji huyo wa Paris Saint-Germain atashiriki Kombe lake la tatu la Dunia siku chache zijazo, ambapo atakuwa akitafuta kuiongoza Brazil kwa ushindi wao wa kwanza kwenye michuano hiyo kwa miaka 20.


Neymar atakuwa na umri wa miaka 34 wakati Kombe la Dunia la 2026 linaanza, na kwa uhakika mdogo kama atashiriki katika michuano hiyo, anatumai kuimarisha nafasi katika historia ya soka kwa kuiongoza Brazil kutwaa taji hilo nchini Qatar.

Neymar aliiambia Globo; “Nitacheza kama ni la mwisho, ninazungumza na baba yangu, huwa tunazungumza na nitacheza kila mchezo kana kwamba ni wa mwisho kwasababu hujui kitakachotokea kesho.”

Neymar: "Qatar Inaweza Kuwa Kombe Langu La Mwisho"

Aliongezea kwa kusema kuwa hawezi kuhakikisha kwamba atacheza Kombe la Dunia lingine hivyo atacheza kama fainali huku akisema kuwa kutakuwa na mabadiliko ya mwalimu baada ya Tite kuondoka na hajui kama ataipenda.

Mchezaji huyo tayari amejenga historia ndefu katika timu ya Taifa na kwa hakika, anataka kumaliza vyema. Mchezaji huyo ana furaha kwani anapenda mpira na kile anachokifanya huku akisistiza kuwa bora muda wote.

Alipoulizwa kuhusu nafasi ya Brazil ya kufuzu Qatar, Neymar aliongeza: “Nataka kucheza kombe hili, kujitolea kwa hilo, kwa sababu nina uhakika tuna uwezo wa kufika mbali sana, ingawa watu wengi hawatuamini, tutathibitisha vinginevyo”

Tangu aanze kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika ardhi ya nyumbani mwaka 2014, Neymar amehusika moja kwa moja katika asilimia 42 ya mabao 19 ya Brazil kwenye michuano hiyo (mabao sita, asisti mbili).

Neymar: "Qatar Inaweza Kuwa Kombe Langu La Mwisho"

Wakati huohuo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amefunga mara 75 katika mechi 121 alizoichezea Brazil, na hivyo kumfanya apunguze mabao mawili pekee ya rekodi ya Pele ya Selecao ya 77.

Ingawa Neymar atatarajiwa kusumbua rekodi hiyo wakati Brazil itamenyana na Serbia, Uswizi na Cameroon katika kampeni ya Kundi G huko Qatar, anasema hasukumwi na hamu ya kufanya vyema zaidi kwa Pele.

Neymar: "Qatar Inaweza Kuwa Kombe Langu La Mwisho"

Neymar alisema kuwa ni zaidi ya alivyowazia kuliko alivyoota, na hakuwahi kufikiria kuhusu namba, hakuwahi kutaka kumpita mtu yeyote au kuvunja rekodi bali siku zote alitaka kucheza soka. Aliongeza kwa kusema kuwa Pele ndiye rejeleo, Pele ni mpira wa miguu, Pele ni kila kitu kwa nchi yetu, na heshima na pongezi zlizonazo kwake ni kubwa sana.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa