Christian Pulisic amesema kuwa lazima Marekani ijivunie juhudi zao kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar na Taifa hilo lisijisikie vibaya tena kwa kutolewa katika hatua ya 16 bora.

Kichapo cha 3-1 kutoka kwa Uholanzi kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa mjini Doha kiliifanya Marekani kutupwa nje ya michuano hiyo hapo jana, na sasa Marekani wanatakiwa kuelekeza katika kukuza kikosi chao changa zaidi kabla ya Kombe la Dunia la 2026.
Mashindano hayo yataandaliwa pamoja na Marekani, Kanada na Mexico, na kushirikisha nchi 48, na Pulisic anataka kuona timu iliyo na ubora wa kushinda mataji, huku akisisitiza kuwa kwasasa ni ngumu tu, unajua inauma baada ya hasra ngumu kama hiyo, wanahisi kama wangeweza kupata zaidi.
Pulisic anasema kuwa ni tukio lingine kwa watu hawa wote, wakati wanaweza kujivunia hawataki kujivunia hivi tena na wanataka kujiweka katika nafasi ya kushinda mashindano kama hayo.

Pulisic alikosa fursa nzuri ya kufungua ukurasa wa mabao dakika tatu kabla ya mchezo, kinyume chake Memphis Depay aliitumia nafasi vizuri na kupachika bao la kwanza, huku naye Blind akifanya matokeo kuwa 2-0 hadi muda wa mapumziko.
Mchezaji huyo wa klabu ya Chelsea anasema kuwa walijilinda vyema kwa sehemu kubwa, lakini walikuwa chini tayari kwa mbao mawili na haikutakiwa hivyo, wakati kocha wa USA Gregg Berhalter anakaribia mwisho wa mkataba wake, hakutoa ufafanuzi zaidi juu ya mustakabali wake.

Antonee Robinson, hata hivyo, anatumai Berhalter anaendelea na jukumu hilo huku Marekani ikitazamia kujijenga kuelekea 2026. Beki huyo wa pembeni wa Fulham amesema kuwa vijana wengi wana nafasi ya kujiendeleza na kundi hilo, na anahisi kama wakati huu wote wameonyesha aina ya soka wanayoweza kucheza.

