Kiungo wa kati wa Ufaransa Aurelien Tchouameni hajashtushwa na kushughulikia majukumu ambayo kawaida huwekwa kwa nyota waliojeruhiwa Paul Pogba na N’Golo Kante baada ya kuisaidia Les Bleus kutinga fainali ya Kombe la Dunia.
Kikosi cha Didier Deschamps kiliishinda Morocco kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Al Bayt hapo jana na kujihakikishia kucheza fainali ya pili mfululizo dhidi ya Argentina siku ya Jumapili.
Ushindi huo wa jana umeifanya Ufaransa kuwa Taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mfululizo tangu Brazil mwaka 2002 kwani walifanikiwa kumaliza mbio za Morocco.
Tchouameni alipoulizwa kama nafasi ya Pogba au Kante inamfaa zaidi alijibu; “Ni zote mbili na wakati mwingine ni kazi yangu kurejesha baadhi ya mipira kama leo, na wakati mwingine nina nafasi ya kufunga bao, kama mchezo uliopita.”
Aliongeza kwa kusema kuwa Pogba na Kante ni wachezaji wazuri kwao na kwa bahati mbaya hawapo hapa kwasababu ni majeruhi kwahivyo wanajaribu kufanya kila wawezalo kuisadia timu katikati ya uwanja, na anadhani wanafanya kazi kubwa.
Kando na Fofana, Tchouameni alikuwa sehemu ya uoanishaji wa viungo wasio na uzoefu, lakini Deschamps anaamini kwamba wote wamethibitisha kuwa wanafaa katika kiwango hiki.
Akisema kuwa; “Uzoefu sio kila kitu, wana sifa nzuri na wanacheza na vilabu vya juu, na huenda hawana uzoefu mkubwa katika kiwango cha Kimataifa, lakini wanatosha kucheza katika kiwango hiki wana uwezo mkubwa, ubora wa hali ya juu na wanaungwa mkono na wachezaji wazoefu wanaowazunguka.”
Deschamps aliongeza kuwa ni kweli kuna nafasi ya kuimarika, lakini ana nguvu zote za kufanikiwa katika kiwango hiki, na hakuwa na shaka kuwachezesha wote wawili pale, inagwa kwa vile walikuwa na wachezaji wazoefu karibu nao.